JANA USIKU JESHI LA POLICE ZANZIBAR, LILITOA AGIZO HILO LIKIITAKA JUMUIYA IYO KUSIMAMISHA MUHADHARA WALIKUA WAUFANYE LEO MAENEO YA LUMUMBA NA MAENEO MENGINE,LAKINI
KWA MSISITIZO WANAMUAMSHO HAO WAMESISITIZA KUENDELEA NA MIHADHARA YA KUZINDUANA JUU YA HATMA YA NCHI YAO ZANZIBAR, MPAKA PALE ZANZIBAR ITAKAPO PEWA MAMLAKA YAKE(MUUNGANO KUVUNJWA)..
NA KWA SASA WAPO MSIKITI WA MBUYUNI WANAENDELEA NA MUHADHARA WALIYOUKHAIRISHWA LUMUMBA KWA SABABU ZA KIUSALAMA NA KUSISITIZA MPAKA UVUNJIKE....
Hivi hawa jamaa wametumwa au
Hivi kumbe hata Mh rais Jakaya kikwete anafahamu kuwa uamsho ni wahalifu hebu soma sehemu ya hotuba yake
Ndugu Wananchi;
Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kwamba, wenzetu hawa wamefanya uhalifu huo kwa hoja ya kupinga Muungano. Haiwezekani mtu anayepinga Muungano, akaitetea hoja yake kwa kuchoma moto makanisa au kuvunja maduka ya watu na kupora mali zao. Ukristo haukuingizwa Zanzibar na Muungano, bali ulikuwepo karne kadhaa kabla ya Muungano na wala haukutokea Tanzania Bara. Na kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais Ali Mohamed Shein jana, ukweli ni kwamba, dini ya Kikristo kama ilivyo ya Kiislamu imeenezwa Bara kutokea Zanzibar. Kanisa kuu la Anglikan Zanzibar lilijengwa kuanzia mwaka 1873 na lile la Katoliki kuanzia 1893 ni miongoni mwa Makanisa makongwe kuliko mengi kama siyo yote kwa upande wa Zanzibar na Bara.
Katika hotuba yake ya jana, Mheshimiwa Rais, Dkt. Ali Mohamed Shein,pamoja na kueleza kwa ufasaha ukweli huu, pia alisisitiza suala la haki na uhuru wa Kikatiba wa mtu kuchagua au kubadilisha dini au imani yake. Katika kutumia uhuru huo, mtu hastahili kuingiliwa au kulazimishwa na mtu yo yote. Hayo pia ndiyo matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kweli yanayofanywa na ndugu zetu wa Uamsho ya kuchoma moto makanisa siyo sawa hata kidogo. Na, wanapoyafanya kwa kisingizio cha Muungano ni jambo lisiloeleweka kabisa na wala halina mantiki. Labda wenzetu wana lao jambo
Huu ni mkanganyiko unaohitaji maelezo na vitendo mh rais la sivyo wa Tanganyika watasimama na kudai
nchi yao pia..
Kuna msemo kwenye facebook kuwa nyumba ya mganga haikosi nyimbo sasa je hii ndio nyimbo mpya ya nyumba ya mganga.!!!!
No comments :
Post a Comment