Bwana asifiwe nawasalimu wote katika Jina la YESU,Natumaini
wote ni wazima na chukua fursa hii kuwaomba msamaha kwa kutoweka hewani kwa
kipindi kirefu hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wangu.
Leo nakuletea segment
mpya kabisa inaitwa kitaalaamu zaidi aka
kiufundi zaidi na kwenda moja moja
kuzungumzia ubunifu katika kuimba.Miaka ya hivi karibuni hapa nchini kumeibuka
waimbaji wa wa aina mbalimbali hilo sio
tatizo, tatizo ni namna wanavyoimba na kutunga ndo loh yaana hakuna ubunifu kabisa
rose muhando |
Wenzetu wa south Africa ambao sasa wamekua kwa kiasi kikubwa tunawaiga sio kwamba
wanajua kuimba sana ila ni wabunifu katika uimbaji wao mchukulie mfano solly
mahlangu yaani akikanyaga jukwaa huta tamani ashuke kwa namna anavyoimba na
kutawala jukwaa kwa ubunifu wa hali ya juu.cheki na uche japo yeye ni mnegeria
lakina nyimbo anazoimba zinakua na mvuto wa tofauti kwasababu kuna ubunifu wa
hali ya juu .
joyous celebration 14 |
solly mahlangu mzee wa obligado,mwamba mwamba |
Hivi ukiulizwa asili ya nyimbo zetu ni zipi utajibuje?sebene
au kwaito au rumba maana sisi hatuna identity yetu kazi yetu ni kuiga na kufuata
mkumbo ni mtindo gani unahit then tunafuatisha huko kama ni sebene basi woote
tutaimba sebene hata kama hatuna sauti za kuimba sebene au kama kwaito basi
wote kwaito au kuiga vibwagizo vya watu na nyimbo mfano my GOD is good,double
double, nanyingine nyingi.
uche mzee wa double double |
Sisi watanzania
kwanza hatuna muda wa kufanya utafiti wa kutosha juu ya uimbaji
wetu,hatuna mazoezi ya kutosha ,na hatuna muda wa kutathimini na kujifunza na hatuna watu wa kutushauri,kukosoa na hakuna
ushirikiano hivyo tunafanya mambo kwa kujisikia na kazi zetu hazifanyi vizuri
john lisu |
Kwanini tusitunge vibwagizo vya kwetu vya ubunifu kwa nini
tusitunge nyimbo za ubunifu ambazo hata watu wa mataifa mengine yataiga kutoka
kwetu.kama tungeuuliza uche una tumia muda,akili na upako kiasi gani kutunga
nyimbo zako na vibwagizo sijui kama wewe ujngeendelea kujiita muimbaji.Joyous
celebration hutumia miezi mitatu mpaka sita kuanadaa albam moja maana yake hua
wanakaa kujadili,wanarekebisha,wanatengeneza namna yakupiga mziki ndo maana
kitu kina toka bora
miriam lukindo wa mauki mamaa kinyonga |
don moen |
Kuwa mbunifu inawezekana kabisa timiza wajibu wako
muimbaji!!!!!
No comments :
Post a Comment