Thursday, May 31, 2012

STEVEN KANUMBA..MKALI WA FILAMU ALIYEPOTEA GAFLA!!!!



Kila siku ya ijumaa katika blog hii itakua inazungumzia tasnia ya filamu hapa kwetu tz,africa na ulimwengu
kwa ujumla.Na siku ya leo tunaanza kwa kukuletea mtu ambaye kiukweli amechangia sana kukuza na
kuendeleza soko la filamu Tanzania na huyu si mwingine bali ni Hayati steven kanumba.

Nini kimemuua Kanumba?
                hayati kanumba the great
Leo sitaki kuzungumzia kuhusu jamaa alikua ni FM au Akudo au alikufa kwa nini sio hoja ya leo kuu la leo
ni mchango wake katika tasnia ya filamu Tanzania  japo jamaa amefariki lakini mchango wake ni mkubwa na si rahisi kusahalika kwa wasanii kwanza na hapa wapenzi wa bongo movie.Walipotoka na johari akiwa na swaiba wake Ray na johari watu hawakuwapokea vizuri lakini kwa kadili walivyo kuwa wanaendelea ndivyo walivyokuwa wanajizoelea mashabiki wengi na kuwavuta wengine wengi kuingia katika game la filamu.

hayati kanumba akiwa new york akinunua vifaa vya kazi

Mpaka mauti inamkuta kanumba alikua anamiliki kampuni yake ya filamu iliyoitwa kanumba the great na kiukweli kazi zake sasa zilikua zinakwenda kimataifa hasa filam ya devil kingdom aliyofanya na ramsey nouah wa nigeria.Kama jamaa angeachiwa fulsa ya kuishi basi angefanya makubwa zaidi na kuipeleka tasnia hii mbali zaidi.

      kushoto ramsey akiwa na hayati kanumba


       kanumba akiwa na anti ezekiel 

Kazi ambayo yeye mwenyewe alikua akiikubali namna alivyocheza ni crayz love ambapo aliigiza kama chizi.
Miongoni mwa watu walioibuliwa na kanumba ni pamoja na anti ezekiel,uwoya,patcho mwamba,wema,partic, wengine wengi tu jamaa ameacha footstape katika tasnia ya bongo movie.Hata kama vitu alivyokua navyo ni vya misaada lakini juhudi zake zimeonekana na ataendelea kukumbukwa na wadau wa filamu.

                   cover ya devil kingdom
Kwasababu mimi sio MUNGU na sitaki kumlaza mahali pema au pabaya wacha tu ni seme  Mungu amlaze mahali panapo mstahili kwa yale aliyoyafanya ameni
Continue Reading...

Wednesday, May 30, 2012

RUSHWA NA TRAFIC NI BIASHARA MPYA ???

Siku hizi trafic kukusimamisha na kukuomba rushwa ni jambo la kawaida na limekua kama biashara
kwa sasa na mtandao wake ni mkubwa sana maana nimesikia hawa polisi wadogo hupeleka hesabu kwa mabosi wao.Swali la kijiuliza  je takukuru hawalifahamu hilo au hata wenyewe wanahusika na hilo
huku kwetu kibaha kuna maeneo matatu maarufu kwa trafic wala rushwa eneo la kwanza ni mizani ya kupima mizigo.bwawani na stendi ya mailmoja.Polisi wanachukua rushwa wazi wazi watu wa malori na mabasi kila wakipita lazima watoe 2000 mpaka 10000 na ikifika saa kumi jion hata polisi wa kawaida utawakuta wanasimamisha magari utadhani na wao ni trafic cha kuchekesha hawajui hata sheria za barabara

Hali hii itaisha lini kama maisha ni magumu ni kwa kila mtu sio polisi peke yao.Wanao husika watusaidie kwa hili jamani ni keroooooooo,
Continue Reading...

Monday, May 28, 2012

NI FOF IJUMAA HII KITU KATIIIII!!!

Ni ijumaa ya wiki hii yaani tarehe 1/6/2012 wakati tukio linalozidi kushika kasi la Friends on Friday maarufu FOF litakapochukua nafasi yake  mahali pale pale kwa siku zote tamali hoteli majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni mpaka saa tano usiku,wajanja wanajua ninacho maanisha sioya kukosa kabisa mtupio ni gold

nauli kama kawaida 15000 tu fika bila kukosa KITU KATI
Tukutana pale wakati tuna ugawa  mwaka huku tukipata mziki live,dinner.motive inpiration huku tuki have fun
na kupata marafiki wapya
Continue Reading...

Followers