Thursday, May 31, 2012

STEVEN KANUMBA..MKALI WA FILAMU ALIYEPOTEA GAFLA!!!!

Share it Please


Kila siku ya ijumaa katika blog hii itakua inazungumzia tasnia ya filamu hapa kwetu tz,africa na ulimwengu
kwa ujumla.Na siku ya leo tunaanza kwa kukuletea mtu ambaye kiukweli amechangia sana kukuza na
kuendeleza soko la filamu Tanzania na huyu si mwingine bali ni Hayati steven kanumba.

Nini kimemuua Kanumba?
                hayati kanumba the great
Leo sitaki kuzungumzia kuhusu jamaa alikua ni FM au Akudo au alikufa kwa nini sio hoja ya leo kuu la leo
ni mchango wake katika tasnia ya filamu Tanzania  japo jamaa amefariki lakini mchango wake ni mkubwa na si rahisi kusahalika kwa wasanii kwanza na hapa wapenzi wa bongo movie.Walipotoka na johari akiwa na swaiba wake Ray na johari watu hawakuwapokea vizuri lakini kwa kadili walivyo kuwa wanaendelea ndivyo walivyokuwa wanajizoelea mashabiki wengi na kuwavuta wengine wengi kuingia katika game la filamu.

hayati kanumba akiwa new york akinunua vifaa vya kazi

Mpaka mauti inamkuta kanumba alikua anamiliki kampuni yake ya filamu iliyoitwa kanumba the great na kiukweli kazi zake sasa zilikua zinakwenda kimataifa hasa filam ya devil kingdom aliyofanya na ramsey nouah wa nigeria.Kama jamaa angeachiwa fulsa ya kuishi basi angefanya makubwa zaidi na kuipeleka tasnia hii mbali zaidi.

      kushoto ramsey akiwa na hayati kanumba


       kanumba akiwa na anti ezekiel 

Kazi ambayo yeye mwenyewe alikua akiikubali namna alivyocheza ni crayz love ambapo aliigiza kama chizi.
Miongoni mwa watu walioibuliwa na kanumba ni pamoja na anti ezekiel,uwoya,patcho mwamba,wema,partic, wengine wengi tu jamaa ameacha footstape katika tasnia ya bongo movie.Hata kama vitu alivyokua navyo ni vya misaada lakini juhudi zake zimeonekana na ataendelea kukumbukwa na wadau wa filamu.

                   cover ya devil kingdom
Kwasababu mimi sio MUNGU na sitaki kumlaza mahali pema au pabaya wacha tu ni seme  Mungu amlaze mahali panapo mstahili kwa yale aliyoyafanya ameni

No comments :

Post a Comment

Followers