Monday, June 9, 2014

exclusive FROM FACEBOOK NA DR SAMWEL SASALI

Share it Please
Linapofika suala la ndoa hapa Bongo kila mtu ni Mshauri na Kila mtu anasema lake. Kwakuwa kila mtu anasema lake wacha na Mimi niweke Yangu ambayo mimi kwangu niliamini na nina amini kuwa yananisaidia pia katika kujenga familia yangu.

Biblia inasema "Kama Msingi Ukiharibika Mwenye Haki Atafanya Nini". Wakati wa Matayarisho ya |Watu Kuoana wengi tuna Concentrate na "Harusi" na Kusahau Maandalizi ya "Ndoa" Wanayoanza kuijenga wengi wana poteza muda katika Kuvaa, Kula, Kunywa, Ukumbi, Rangi, Mc na kusahau hayo yote ni mambo hayazidi masaa matano na Kusahau Maandalizi ya Ndoa wanayotaka ifanya. Ndoa Ili iweze kusonga ina sehemu kubwa sana ya Kujiandaa kwenye ulimwengu wa Roho kuliko suti na Mashela. Shetani kati ya maeneo anapiga mojawapo ni ndoa ukiwa Single huwezi jua hili ila sarakasi nyingi sana unaweza kuta mnapigwa halafu hamjui tatizo liko wapi, mnaweza kuta tu hamuelewani yaani jambo dogo zogo lake sii lakawada halafu mnatafuta sababu hasa ya kugombana hamuioni, unaweza kuta issue ya hela kwenu ndo huwa inachafua hali ya hewa kila mnapoanza kuongelea.

Unaweza shangaa mumeo ama mkeo alikuwa mtu mzuri tu ghafla hapo kati kabadilika kaanza na michepuko badala ya kujua shetani kapitia wapi mnaaza ugomvi ambao badala ya kuwaunganisha ndio unawaweka mbali. Kuna watu wanachepuka na hawajui kwanini wanachepuka unakuta neno amani kwenu linakuwepo wakija wageni ila wakiondoka ni machafuko kwenda mbele wakati mwingine watu wanatamani kutoka lakini wanaona aibu sababu harusi ilitumia hela nyingi, ama wazazi watawaonaje, ama pengine hadhi zenu na mambo kadha wa kadha mnajiuliza sana haya mambo yanatokea wapi kumbe mlikosea wakati wa kujenga Msingi. Unajikuta wewe ni Mteja Mzuri waChriss Mauki na unafanya yote anayyofanya kumbe issue mwanangu ni Msingi ulioutengeneza katika ulimwengu wa roho. Ukifahamu "Hila" za adui ni rahisi kupambana kuliko ubora wa silaha ulizonazo.

Marafiki zangu wanaotarajia kuoa hivi karibuni yako mengi mtafundishwa lakini pia nami niwape machache ya kuwasaidia.

1. Nani Anasimamia Harusi Yenu (Bestman na Matron). Kila mtu anachaguo lake na vigezo vyake anapochagua Wasimamizi. Wengine wanachagua marafiki zao, wengine wanachagua watu wanaofanafanana, wengine wanachagua wenye hela, wengine wanachagua washikaji. Wasimamizi ni Watu Watakaosimama na nyie siku zote a maisha. Kuna watu kwa ajili ya maendeleo hawataki Wasimamizi well and good.

Samilembe tulichagua Bestman na Matron ambao kwanza ndoa yao inanishawishi kuwa iko stable hata kama inayumba basi bado wako imara, mtu ambaye atatuombea tutakapokuwa tunapita katika mapito mbalimbali, mwenye ushawishi mwingi wa rohoni kuliko muonekano watu tunaowaamini sana katika Imani. Mbili tulichagua watu watakaoweza Kutukemea ama kutofokea zinapofika serious issue. Ukitafuta mshikaji unaweza kuna serious issue mkaisolve kishikaji baadae. Ukipata mtu ambaye kwanza mnaheshimiana, anaweza kukuita na kukukemea, Ukipata wa kukuchekea mtachekea mpaka ndoa yenu inakufa. Tatu tulitafuta mtu ambaye ni Rafiki Yetu mtu ambaye ni rahisi kumwambia issue sensitive na akaelewa. Ukiletewa tu bestman na matron utakuta kuna issue kumbe una hofu nazo sana na huna wa kumwambia. Kuwa makini unapochagua askari mtakaokuwa mnapigana wote vita. Kama vipi sio lazima tafuta tu mshikaji, mlevi mwenzio ila kunasiku utakumbuka kuwa kuna nyakati unatamani upate mtu ambaye anaweka "Kukusikiliza" "Kukuelewa" na "Kukusaidia" kwetu sisi Mwl. Dr..Mtarajiwa Mathew Mndeme na Mkewe Balozi Mtarajiwa Jacque Mndemewalifikia vigezo. Huyu Mndeme haoogopagi kama ndoa yako ni issue mtafute tu kwa Siri ongea nae.

Wapi mnafungia harusi yenu, Kanisani, Msikitini au Bomani. Kila Madhabahu mnayofungia ndoa yenu mjue kuna Mungu wa Madhabahu hiyo. Na Kitengo Cha Kuunganishwa na Madhabahu hiyo mnampa nafasi Mungu Wa Madhabahu hiyo. Na Kila Madhabahu Ina kuhani anayesimamia madhabahu (Mfungishaji). Kuna watu ambao wao wanaamuaga kwenda kufunga baharini, kwenda kufunga hotelini na wengine nyumbani suala la msingi sana sio wapi ila nani anawaunganisha na anaunganisha kwa spirit ipi. Anayewaunganisha mwisho wa siku huwa anawatakia "Baraka" kuwa makini sana nani wanawaunganisha, nani wanawawekea mikono ya kuwatakia baraka maana huwezi kutoa kitu ambacho huna. Unaweza kuta anayewatakia baraka ni Mzee wa Michepuko anapokuachilia baraka anakuachilia na Michepuko juu yenu. Kama Ndoa yake ni Kimeo ujue nae kuna roho anawaachilia juu Yenu. Mnaunganishwa wapi, nani anawaunganisha matters alot unaweza kuta kuna issue mnahangaika sasa hivi kumbe issue Muungano wenu ni kama Tanganyika na Zanzibar. Kwni unadhani Tanganyika na Zanzibar Muungani wake tatizo nini?tatizo ni "namna" walivyoungana na "Waliotuunganisha". Tatizo linaweza Ibuka baadae sana hata baada ya miaka 50 tatizo "waaliowaunganisha".

3. Sadaka Siku Ya Harusi. Maharusi hakikisha mnabeba Sadaka siku ya Harusi yenu hata kama Mnapounganishwa hakuna huo Utaratibu wa kutoa Ombeni kutoa. Kumbuka ni Kwamba Hamjawahi Kutoa Fedha mkiwa Mume na Mke. Fedha yenu ya Kwanza kama Mume na Mke mnaitoa Wapi?Unaweza kuta mnapata tabu sana sasa hivi issue za hela kwa sababu fedha yenu ya kwanza kabisa mlienda supermarket. Mnashangaa sana sasa hivi fedha yenu mnanunua tu nguo, simu, viatu unashangaa hata kama hujapanga kununua kitu ila ukiingia tu Supermarket yaani lazima utoke hata na Ice scream ili mradi tu uache humo fedha yako. Unajishangaa hivi kwanini unafanya matumizi hujapanga?Kumbe Msingi mlioanza kuujenga siku ya kwnza kabisa. Ukienda Kanisani ama Unakofungia harusi yako beba Sadaka na ikiwezekana Sadaka iliyonona. Wengine huenda mbali zaidi hutoa fungu la kumi Jumla ya Michango ili katika Sadaka ya kwanza ama fedha yao ya kwanza kama Wanandoa waliacha kwa Mungu aliyewaunganisha. Hazina ya Mtu Ilipo ndipo na Moyo wake Ulipo.

4. Nani anakufundisha na Nakufundisha nini Kabla ya Ndoa. Kuna watu wanafundishwa na Ma-Kungwi, Kuna Watu wanafundishwa na Wanasaikolojia, Kuna Watu Wanafundishwa na Ma-Shosti....Ila Ukishikwa yoote unasahau unabaki kusema "Mungu Nisaidie". Humwambii Kungwi akusaidie, Humwambii Shost akusaidie ila kuna Issues Wallah tena Unamuhitaji Mungu Mzima Mzima. Kila neno ama jambo unalofundishwa ujue linabebaa tofali la ujenzi wa ndoa yenu. Ni vema sana mkajua Mungu ndo designer wa Ndoa lazima mjifunze sana kutoka kwenye Neno lake. Mtajifunza tofauti za wanaume na wanawake utajifunza "How to Handle the Disturb-on Husband" na utashangaa unapigwa kila siku. Kuna mambo yanatia hasira kuna mambo yanatia kichefuchefu kuna mambo yanakatisha tamaa. Kabla hujapelekwa kwa shost Mwambie aliyekupa Mume ama Mke. Kama Mke mwema na mume mwema anataoka kwa Bwana sasa kwanini issue zinapotokea unampeleka kwa shost yako?Ukinunua Kiatu Chakula Kibovu Supermart ya Mlimani City Dar....na unayo "Hati" ya Kununulia (cheti na haki ya unganiko) huwa tunarudisha kwa aliyetuuzia na sio kwingineko. Kama Mungu amekupa mbovu mwambie yeye kwanza. Usikubali kuolewa Kibudu "Bila haki ya Unganiko" kuna siku utajikuta unahitaji kuwa na "uhalali" ambao unajikuta huna.

Mambo 6 nitamalizia Baadae.

Kama Msingi Umeharibika Mwenye Haki Atafanya Nini?Ukiwa na Kiherehere cha Kuoa ama Kuolewa kumbuka pia kuna Matofali ya Kujengea ndoa yako. Uimara wa Jengo unapimwa Wakati Wa Dhoruba.

Good Morning Teacher.......
 — with Jacque Mndeme and Milembe John Madaha. (4 photos)

No comments :

Post a Comment

Followers