Wednesday, August 8, 2012

CREATIVITY IN PRAISE AND WORSHIP /SING season 1


Bwana asifiwe nawasalimu wote katika Jina la YESU,Natumaini wote ni wazima na chukua fursa hii kuwaomba msamaha kwa kutoweka hewani kwa kipindi kirefu hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wangu.

Leo nakuletea  segment mpya kabisa inaitwa kitaalaamu zaidi aka kiufundi zaidi  na kwenda moja moja kuzungumzia ubunifu katika kuimba.Miaka ya hivi karibuni hapa nchini kumeibuka waimbaji wa  wa aina mbalimbali hilo sio tatizo, tatizo ni namna wanavyoimba na kutunga  ndo loh yaana hakuna ubunifu kabisa 
rose muhando
 
Wenzetu wa south Africa ambao sasa wamekua  kwa kiasi kikubwa tunawaiga sio kwamba wanajua kuimba sana ila ni wabunifu katika uimbaji wao mchukulie mfano solly mahlangu yaani akikanyaga jukwaa huta tamani ashuke kwa namna anavyoimba na kutawala jukwaa kwa ubunifu wa hali ya juu.cheki na uche japo yeye ni mnegeria lakina nyimbo anazoimba zinakua na mvuto wa tofauti kwasababu kuna ubunifu wa hali ya juu .
joyous celebration 14 

solly mahlangu mzee wa obligado,mwamba mwamba

 
Hivi ukiulizwa asili ya nyimbo zetu ni zipi utajibuje?sebene au kwaito au rumba  maana sisi hatuna  identity yetu kazi yetu ni kuiga na kufuata mkumbo ni mtindo gani unahit then tunafuatisha huko kama ni sebene basi woote tutaimba sebene hata kama hatuna sauti za kuimba sebene au kama kwaito basi wote kwaito au kuiga vibwagizo vya watu na nyimbo mfano my GOD is good,double double, nanyingine nyingi.
uche mzee wa double double
 
Sisi watanzania  kwanza hatuna muda wa kufanya utafiti wa kutosha juu ya uimbaji wetu,hatuna mazoezi ya kutosha ,na hatuna muda wa kutathimini na kujifunza  na hatuna watu wa kutushauri,kukosoa na hakuna ushirikiano hivyo tunafanya mambo kwa kujisikia na kazi zetu hazifanyi  vizuri
john lisu
 
Kwanini tusitunge vibwagizo vya kwetu vya ubunifu kwa nini tusitunge nyimbo za ubunifu ambazo hata watu wa mataifa mengine yataiga kutoka kwetu.kama tungeuuliza uche una tumia muda,akili na upako kiasi gani kutunga nyimbo zako na vibwagizo sijui kama wewe ujngeendelea kujiita muimbaji.Joyous celebration hutumia miezi mitatu mpaka sita kuanadaa albam moja maana yake hua wanakaa kujadili,wanarekebisha,wanatengeneza namna yakupiga mziki ndo maana kitu kina toka bora
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcII2GTfPGqoXIKe9jeWMoihJw_SACZrbS-J07xZDaF9D5pHGrUUYnDDVoaN40agl7b4GBYyYmILnXATXpip0cKfoGkwVWEbOh9JUqEIZ-KwXo2NLD6P5tNXyhB0tP5ib-JJyZsaCvGhU/s400/Miriam.jpg
miriam lukindo wa mauki mamaa kinyonga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijCmMrXIFeOVTajjAMNWF1gAoJSoin2YLy4oAUlBNyN8yIUjoGZVOrLN5vbTIQT5h1XVbdx6IYSPBhNmxAgnrDxZAf7bJaZdVWgNhvDJkFGSqis9Z3-JZs_YPAivPSAVgeBucvzOlqxvr2/s1600/CTC-1862-image4.jpg
don moen
 
Kuwa mbunifu inawezekana kabisa timiza wajibu wako muimbaji!!!!!
Continue Reading...

Followers